Nchi ya Afrika kusini itazindua jumatatu hii sanamu mpya ya rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo aliye zikwa jana mzee Nelson Madiba Mandela mjini Pretoria, kwenye eneo la Union Bulding, jengo ambalo lilitumika kumuapisha Mandela Mwaka 1994 kuwa rais wa Afrika kusini.
Uzinduzi huu unafanyika siku moja baada ya kuzikwa hapo juzi katika kijiji cha Qunu.
Rais wa Afrika ya kusini, Jacob Zuma, atawaongoza viongozi mbali mbali serikalini na familia ya Nelson Mandela kuzindua rasmi sanamu mpya ya Mandela ambayo inatajwa kua kubwa zaidi duniani, na itakua na urefu wa zaidi ya mita 9.
Uzinduzi wa sanamu hii unaenda sambamba na siku maalumu ya hii leo ya upatanishi, kukumbuka tukio la mwaka 1838 ambapo jeshi la Voortrekkers lilipigana na kulishinda jeshi la jamii ya Wazulu.
Katika vita hivyo, watu zaidi ya 100 walipoteza maisha, na baadae jeshi hilo liliondoka kwenye ardhi ya watu kutoka jamii ya Wazulu.
Tukio la pili kwa tarehe hii ya leo ni lile la mwaka 1961, wakati chama cha ANC kiliunda jeshi lake ambalo lilijulikana kwa jina la Umkhonto we Sizwe dhidi ya utawala wa Frederik de Klerk kwa kukabiiana na ubaguzi wa rangi
Siku hii ya mapumziko nchni Afrika ya kusini ilitangazwa rasmi na Nelson Madiba Mandela, baada ya kutangazwa kua rais wa Afrika ya kusini tarehe 10 may 1994.