Elimu, Kuwaezesha na kushawishi ndiyo dhumuni la kipindi cha “Women’s Empowerment Show”, Dhumuni kubwa ni kuwaleta wanawake waliofanikiwa na kutazama wamefanya kipi cha tofauti kwenye jamii na jinsi wanavyoweza kushawishi wengine kufanya hivyo.
Mgeni wa kwanza kwenye kipindi hiki alikuwa Dk. Trish Scanlan ambaye anaendesha kitebgo cha paediatric oncology katika hospitali ya Muhimbili. Toka alipoanza mwaka 2008 , akiwa na timu yake ya madaktari na wakunga wa Tanzania waliojitoa kwa dhati kufanya kazi, kwa muda mchache waliofanya kazi, idadi ya watoto wenye saratani waliopona imepanda kutoka asilimia 12 – asilimia 60.