Chriss Brown na Drake walipanga kuachia ngoma yao mpya Jumatatu huko Toronto Canada lakini mpango huo umegonga ukuta kwa sababu Chriss Brown hawezi kuingia nchini huko TMZ imeripoti.
TMZ waliambiwa Drake alimualika Chriss Brown ajiunge nae Jumatatu kwenye steji wakati wa Tamasha la OVO, TMZ wameambiwa kwamba Chriss alikubali na mpango ulikuwa kwa wasanii hao kuperform ngoma ambayo wameshirikiana pamoja ambayo waliifanya mwezi uliopita.
Show hiyo ingekuwa kubwa sana kwa sababu kuu mbili, ni mara ya kwanza wakali hao wangeperform pamoja na katika ngoma hiyo wote kila mmoja amemtaja Rihanna kwa aina yake.
Ugumu upo kwa sababu Chriss Brown asingeruhusiwa kuingia Canada, kwa sababu nchi hiyo huwa haivumilii kabisa kwa wahalifu kuingia nchini humo, Chriss Brown sio tu an makosa pia amekuwa mkosaji mara kwa mara hata hivyo watu wa Chriss B walitoa habari kwamba hata wakifanya juhudi ili show ifanyike haitakuwa na matunda yeyote.