
“Itakuwa muda fulani pale unapoweza kupata risasi chache, lakini kama unaweza kupona kutoka kwenye kupigwa risasi, inatakiwa ujiweke imara zaidi” alisema Suge Knight.
Suge Knight anasema hajishughulishi ni nani alimpiga risasi tarehe 24 Agosti 24 katika club ya usiku inayoitwa 1-OAK huko Magharibi mwa Hollywood, California.
“Hata kama ningetaka kujua, sidhani kwamba ni muhimu kujua, mtu aliyenipiga risasi, nadhani naendelea vizuri sana, nafuraha hali yangu kuwa nzuri na chochote kinachotokea, kinatokea” alisema Suge Knight wakati akipiga stories na TMZ.
“Nilipigwa risasi ndani ya club na kitu ambacho kila wakati baba yangu aliniambia, haijalishi ni kitu gani, usikate tamaa, Usiache kitu unapoanzisha kitu, kama unapitia kitu, usijali kinachoendelea, wewe yaache sawa kama mtu, nilipigwa risasi, nadhani ilkuwa muhimu kwamba nilitaka kutembea kuhakikisha nafika sehemu salama, ili niweze kuziba matundu ya risasi” aliongeza suge Knight.
Kwa sasa Suge Knight anaendelea kuuguza majeraha ya risasi.
