Ni Saudia Arabia na Utamaduni wao wa bibi harusi haonekana mpaka siku maalum umewatokea puani atii
Ni utamaduni wa Saudi Arabia kwa wanawake kufunika au kuficha sura zao na ushungi au veil Kabla ya harusi hiyo iliyofanyika katika jiji la Medinah, bwana harusi alikuwa hajawahi kuiona sura ya mchumba wake.
Baada ya kufunga ndoa, na wakiwa katika sherehe za harusi, bibi harusi alifunua ushungi ili mumewe aione sura yake kwa mara ya kwanza, na kupiga picha ya pamoja. Alipofunua ushungi na kutabasamu, mumewe alihamaki na kusimama sababu sura ya mwanamke huyo ni mbaya na si kama alivyotarajia. Mwanaume huyo akasema “Sitaki uwe mke wangu. Muonekano wako si kama nilivyotarajia, samahani lakini nakupa talaka.”
Kwa mujibu wa gazeti la nchini humo la Okaz, bibi harusi alianguka chini na kuangua kilio. Wageni waliingilia kujaribu kusuluhisha maharusi, na kumfariji bibi harusi.
“Bwana harusi amesema kuwa hajawahu kuiona sura ya mchumba wake kabla ya harusi.” Liliandika gazeti hilo. “Alipompa talaka katikati ya sherehe ya harusi, sherehe ilikeuga kuwa usiku wa machozi.”