
Baada ya tuzo za BET alisikika Nick Minaj akiua mademu ambao ambao wanaandikiwa ngoma, akasema inatakiwa waandike wenyewe na vitu kama hivyo, kwani pia wanawake wanaweza kuandika na kutisha, akamsifu Miss Eliot, Lauryn Hill na wengine kwani wamekuwa wakiandika na wenyewe na ngoma kufanya fresh.
Hili dongo ilionekana kama linakwenda kwa mwanadada ambae anangoma yake inasumbua kwa sasa ya “Fancy” Iggy Azalea.
T.I akipiga stories na Bijou Star TV alifunguka mambo kibao kuhusu yeye kuendelea kama msanii na kujiwakilisha, anataka watu wapate wapate na kujifunza vitu vipya na kupenda kuhusu yeye, kama msanii inatkiwa ukue msanii unajiongeza wewe kama mtu, mtu lazima ukue, kama msanii haitabariki, unachokiona ni yeye, unchosikia ni yeye hataki kuigiz kitu ambacho hawezi kukiendeleza.Alisema T.I.
Ukiachana na hilo T.I aliongelea kuhusu uvumi kwamba anamuandikia mashairi msanii mwenzake Iggy Azalea.
T.I alisema anaandika ideas zake mwenyewe na mawazo yake, lakini wasanii wanapokuwa studio huwa wanasaidiana labda unamwambia mwenzako hapo unafanya hivi hiyo yote ni katika kuelekezana lakini awezi kuandika kitu anachokuwa akikiwaza Iggy Azalea ni msaada kidogo tu wa kawaida ambao wasanii wanasaidiana wanapokuwa studio.
“Na maana, simuandikii, Iggy ana ideas zake na mawazo yake anawakilisha kivyake, siwezi nikaweka mawazo yake na ideas kwenye maneno namsahihisha tu, anayo aina tofauti ya kujiwakilisha yeye na sanaa yake, msinielewe vibaya vibaya, studio kila mtu anasaidia viunganishi na vitu kama hivyo, hivyo ndivyo inavyokuwa kwangu na hata top 5 ya marepa wengine unataka ideas kali” alisema T.I.
Kwa sasa Iggy ameshirikishwa na T.I kwenye ngoma yake mpya inayoitwa “No Mediocre” na katika mahojiano hivi karibuni kwenye kituo cha Powr 106 na Big Boy Neighborhood kiongozi huyo wa Grand hustle T.I aliongelea jinsi alivyomgundua Iggy mwanadada kutoka Australia uwezo wake wakati anaanza.
