Wakati Bobbi Kristina Brown akipigania uhai wa maisha yake katika hospitali iliyopo Atlanta, kuna sehemu za mwili wake imeripotiwa kwamba havifanyi kazi, mwanasheria wa familia ya Brown amekemea taarifa kwamba binti huyo mwenye umri wa miaka 21 Bobbi Kristina atatolewa mashine inayomfanya aishi ndani ya siku chache zijazo. Wakati huo huo, polisi wa Roswell Georgia, mji ambao alikutwa ameanguka nyumbni kwake akiwa hajifahamu kwenye bathtub Januari 31, polisi wanajaribu kutafuta kilichopelekea star huyo kukutwa na hali hiyo MAENDELEO MATANO YA HALI YA BOBBI KRISTINA KWA SASA Mwanasheria wa familia ya Brown akemea ripoti zinazotolewa kwamba Boobi Kristina atatolewa mashine inayomfanya aishi wiki hii, Siku 16 baada ya binti wa Bobby Brown na marehemu Whitney Houston alipokimbizwa hospitali na kuwekewa mashine, ripoti zimeendelea kuzunguka zikisema kwamba familia hiyo ambayo imechanganyikiwa kwa sasa wanampango wa kuondoa mashine inayomfanya aishi wiki hii. Lakini mwanasheria wa Bobby Brown Christopher Brown alitoa taarifa fupi kwa vyombo vya habari akisema kwamba zilizoenea ni habari za uongo, hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na hali ya Bobby Kristina. VIUNGO VYA MWILI WA BOBBI KRISTINA IMESEMWA KUTOFANYA KAZI Hali ya Bobbi Kristina ilikuwa mbaya wikiendi iliyoisha na sehemu za mwili wake iliripotiwa
kuanza kuacha kufanya kazi, ingawa maendeleo haya mabaya, watu walio karibu na Bobbi Brown wameambia baadhi ya vyombo vya habari kwamba waendelee kuwa na tumaini kwamba binti wake atapona na anataka aendelee kukaa kwenye mashine.
RAFIKI WA BOBBI KRISTINA AMAINDI KWA KUZUILIWA KUMTEMBELE Katika mahojiano yaliyorushwa na Februari 12, ndugu yake Bobbi Kristina Jerod Brown aliiambia kituo cha televisheni cha Atlanta kwamba familia yake imemkataza boyfriend wake Nick Gordon kwenda kumtembelea hospitali. Jerod alienda mbali zaidi akisema Gordon anafungua kesi kwanini ananyimwa kumtembelea Krissy kwa sasa akiwa hospitali. Lakini timu ya kisheria ya Gordon imesema sio haraka sana katika kujibu ripoti kwamba Nick Gordon anafuatilia kisheria, atapenda haya yamalizwa, hataki kupeleka mambo katika vyombo vya sheria, wanasheria wake Randy Kessler na Joe Habachy walisema katika maelezo kwamba suala kubwa analotaka Gordon ni kupona tu kwa Bobbi Kristina. Wakati huo huo Februari 15, Gordon alibadilisha picha yake ya ukurasa wa twitter na kuweka tattoo aliyoandika jina la Bobbi Kristina kwenye mkono wake na aliwaambia followers kwamba anashukuru kwa kumtakia Bobbi Kristina mazuri apone. Aliandika “asanteni kwa maombi yenu yote, ni mtu aliye imara na atapona, endelea kumuombea” alitweet Gordon KUZAMA KWAKE IMEANZISHA UCHUNGUZI MKALI Wapelelezi walisema kwamba wanasumbuliwa na vidonda alivyokuwa navyo Bobbi Kristina kwenye uso na mdomoni, na ripoti fulani zilitoka kwenye vyombo vya habari vikimuhusisha Gordon kuhusika na majeraha hayo. Polisi walithibitisha, wanachukua suala hilo kama kosa la jinai, na mwanasheria wa Bobby Brown ameongeza huu ni uchunguzi wa kosa la kijinai na ukweli wa suala hili unahitaji utulivu mkubwa. MAOMBI YAENDELEA, ZIKIIMBWA NYIMBO ZA MAMA YAKE NA MACHOZI KUTAWALA Siku ya hisia Februari 9 iliyofanyika Riverdale Georgia, walionekana marafiki, mashabiki, wanasiasa wakituma maombi kwa Bobbi Kristina. “Sahau kwamba Bobby Brown ni msanii anayejulikana, marehemu Whitney Houston alikuwa ni msanii anayejulikana pia, bado ni watu, wanatoka damu na wanaumia kama sisi” alisema Mayor wa Riverdale Dr. Everlyn Wynn-Dixon wakati wa tukio hilo. Mawaziri mbalimbali walihutubia umati wa watu na kutoa maneno ya kutia moyo, “tuko hapa kuwainua watu, na kuendeleza maombi yetu ndicho kinachohitajika kwa muda huu, tukio hilo lilipokuwa likifika mwishoni mwanamuziki mkongwe wa R&B Tony terry aliimba wimbo wa “I look to you” wimbo alioimba Whitney mara ya mwisho ikiwa na anarudi katika gemu kabla ya kifo chake 2012. Jinsi Terry alivyokuwa akiendelea kuimba aligusa mioyo ya umati uliokuwa umekusanyika na kuwafanya watokwe na machozi.