Wakati tukiwa tunasherehekea miaka 52 Ya uhuru wa Tanzania yetu bado hali ni mbaya huko vijijini ambapo swala la miundombinu na zahanati ni kitendawili, hali hiyo imedhihirika baada ya mama mmoja huko Songea ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa Haraka kujifungulia njiani wakati anakimbizwa hospitalini kupata huduma ya kujifungua ndipo mambo yakaharibikia njiani kutokana na umbali wa zahanati ilipo na miundombinu yenyewe
Kutokana na kukosekana kwa zahanati na wanawake kutokuwa na elimu ya uzazi kumesababisha mwanamke huyo mkazi wa Masamala Songea Mkoani Ruvuma kujifungulia barabarani
Hata hivyo mama huyo alifanikiwa kijifungua salama na wasamaria wema walijitokeza na kumuwahisha Hospitalini wakiwemo wanawake Wawili Na Dereva Boda Boda Mmoja kwa msaada wa Ki daktari Zaidi
Bado Tunasafari ndefu…