Makardinali wa kanisa katoliki dunia wameshindwa kumchagua Papa mpya katika siku ya kwanza na ya pili ya mkutano wao mjini Vatican.
Makardinali hao wanakutana kwa siku ya pili leo kumchagua mrithi wa Papa Benedict, aliyejiuzulu mwezi uliopita.
Kura zingine zitapigwa baadaye mchana. Moshi mweusi ulionekana ukitoka kwenye paa la kanisa Sistine kuonesha kuwa kura hazijatosha kumpata Papa mpya na wa 266.
Ukitoka moshi mweupe ni ishara kuwa Papa mpya amepatikana.
Baadhi ya wananchi kutoka mataifa mbalimbali duniani wakifualitia kwa ukaribu mkutano huo wa Vatican
Makardanali hao 115 watapiga kura mara nne kila siku hadi theluthi mbili yao wampigie kura mmoja. Miongoni mwa makardiinali wanaotajwa kuwa na uwezekano wa kushika wadhifa huo ni pamoja na Angelo Scola wa Italia, Odilo Scherer wa Brazil na Marc Ouellet wa Canada.