Hii video nilitaka niitoe siku ta tarehe 13 mwezi june siku ambayo ndio tarehe niliyosherehekea miaka mitano ya ndoa yangu kwa bahati mbaya kuna jambo lilitokea hapo kati kati nikashindwa kutimiza kwa siku husika. Ila hakijaharibika kitu… nimefanikiwa kwasasa na nimeweza kukuwekea Video hii ambayo ni clip ndogo tu yenye mchanganyiko wa siku ya Kitchen Part, SendOff Ndoa pamoja na Reception.
matukio yanaonekana kwa mtiririko kama nilivyotaja, kitchenPart yangu ilifanyika Nssf Water Front, SendOff ilifanyika DICC Posta, Ndpa ikafungwa nyumbani kwetu Same Kilimanjaro na reception ikafanyika nyumbani kwa kina mume wangu Kifaru Mwanga Kilimajaro
tarehe 13 ya mwezi wa sita mwaka 2008 ndio siku hasa nilifunga ndoa takatifu katika dini ya kiislam na mchumba wangu wa siku nyingi Abbas Mziray. ukijumlisha miaka ya uhusiano wetu mpaka ndoa unapata miaka tisa sasa tukiwa pamoja miaka minne ya mahusiano ya kawaida na miaka mitano ya ndoa
Happy Anniversary to us.
1 Comment
Ulipendezajeee nitakutafuta unipeleke kwa aliyekupamba