Tukio la kumkabidhi Tuzo msanii bora wa kiume kupitia tuzo za kilimanjaro mwaka huu lilinihusu sana bada ya kutajwa kuikabidhi tuzo hiyo kwa mshindi husika kwa mwaka huu.
Mshindi aliibuka msanii Diamond ambaye hakuwepo ukumbuni hapo kutokana na kutajwa kuwa katika usiku wa kinywaji cha Coka Cola kwa kuwa siku ziligongana na hakuweza kukosa huko kutokana kuwa balozi wa kinywaji hicho na tuzo yake kuchukuliwa kwa niaba yake na Muwakilishi wa waandaaji wa Tuzo hizo za kilimanjaro.