Number One songstress, Wema hubby to be Diamond Platinum amesema hakupanga kuachia video ya wimbo wa “Bum Bum” ambayo amemshirikisha Iyanya hapa Tanzania, lengo lake lilikuwa kuachia nje ya nchi kwa ajili ya kumtangaza huko zaidi kwa sababu maadhi yake yamekaa Kiafrika magharibi zaidi, kwa kifupi ungeanzia nje ndo urudi Tanzania.
Diamond akipiga stories na Dj Tass kwenye Kwetu Flava ya Magic FM jana alisema alikuwa na video mbili ya “Mdogo Mdogo” na Bum Bum” akiwa amemshirikisha Iyanya, Lakini baada ya watu kuiona video hiyo wakaanza kumwambia hii video kali sana yeye hakutegemea kama Wabongo wangeikubali sana kwa sababu target zake zilikuwa ni nje ya Tanzania zaidi.
Baada ya Diamond kuona kumbe hata Wabongo wanaielewa zaidi na wameisifia akaona aichie ndipo akaachia video mbili kwa siku moja, kuhusiana na ngoma ya “Bum Bum” aliyomshirikisha Iyanya ambayo kwa mara ya kwanza ilichezwa kupitia “Kwetu Flava” ya Magic FM alifanya ngoma hiyo ili azidi kujitangaza zaidi Afrika ya magharibi ambako ndipo muziki wa Afrika ulipo, ukijulikana Afrika ya magharibi basi unakuwa unaelekea kuikamata dunia, alianza na Davido kwenye “My number one” ngoma ambayo imemtangaza Diamonda vyema kabisa katika tasnia ya muziki duniani na kupelekea kuingizwa katika kuwania tuzo za MTV na BET.
Diamond amesema kushirikia tuzo hizo ingawa hajashinda lakini amejifunza vitu vingi sana, pia amekutana na watu wengi na network imezidi kuwa kubwa, kushindwa kwake sio yeye tu alishindwa wapo wasanii wengine akubwa tu hawakushinda lakini kuwepo tu pale ni ushindi tosha.
Mkali Ommy Dimpoz nae alizungumzia kuhusu ujio wa wasanii kutoka Marekani ambao walikuja Tanzania ili kuweza kubadilishana mawazo jinsi wao wanavyofanya mpaka wanaweza kufika mbali, Ujio wa wageni hawa ni ahadi ya Rais Kikwete aliyoitoa Dodoma kwamba angeleta wasanii na wataalamu kutoka nje ii waweze kukaa na wasanii wa Kitanzania na kuwaonyesha ni vitu gani wanaweza kufanya ili waweze kufanikiwa zaidi katika sanaa.
Kikubwa alichokisema Ommy Dimpoz alichojifunza katika Semina hiyo ni jinsi ya wasanii kujiuza, kujituma ili uweze kutengeza kazi yenye ubora ambao utakufikisha mbali, kujitangaza kimataifa zaidi, Wasanii wasione kwamba wanajuikana Tanzania basi wajue kila mahali wao wanajulikana inatakiwa kutoka kwenda kujitangaza mbali zaidi.
Katika semina hiyo aikuwepo David Banner kutoka Marekani, Chaka Zulu mwana hip hop mkubwa duniani kutoka Marekania pia na Terrence Jay mtangazaji wa kituo cha E-News.
Kwa upande wa video ya Ommy Dimpoz ya “Ndagushima” iimgharimu paundi 15,000 na maeneo yanayoonekana katika video hiyo ni London nchini Uingereza.
Akiwa kwenye Kwetu Flava Dj Tass aliwauliza Diamond na Ommy Dimpoz wanaoa lini?
Ommy Dimpoz alisema Ramadhan ijayo atakuwa akila ftari iliyopikwa na mke wake na alitakiwa amtaje mchumba wake aligoma, kwa upande wa Diamond yeye mpenzi wake ni Wema na mipango inafanyika iko siku itakuwa wazi harusi ni lini. Tusubiri pia inaweza ikawa couple yenye nguvu Tanzani pia…Good luck…Rais wa wasafi.