Kampuni inayoongoza kwa mawasiliano nchini Vodacom Tanzania na kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola Tanzania wamezindua promosheni ya Coke Studio itakayowawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kupata dakika 5 za maongezi wanapokunywa soda ya Coke ambapo mteja atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wenye namba zilizopo chini ya kizibo kwenda namba 15441. Akiongea katika uzinduzi wa promosheni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam Meneja wa Kinywaji cha Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka amesema ”promosheni hii ni katika kuhakikisha kwamba vijana na wateja wote kwa ujumla wanapata nafasi ya kuburudika na kinywaji cha Coca-Cola, lakini pia kuweza kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kuperuzi kwenye intaneti kwa muda wa dakika 5”
Nae Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa akizungumza katika uzinduzi huo amesema promosheni hii inayojulikana kama Kunywa Coke #Kula5 ina lengo la kuwafurahisha wateja wa Vodacom Tanzania na wenzao wanaowazunguka. ”mteja atakuwa anafurahia kunywa Coke wakati huo pia anapata fursa ya kutumia huduma za mtandao kwa dakika 5 kwa namna yoyote anayotaka yeye (mteja) ikiwa ni kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi au kuperuzi’’
“Mteja wa Vodacom ataunganishwa na huduma hii kwa kupeleka ujumbe wenye namba iliyopo chini ya kizibo cha soda yake ya Coca-Cola ya chupa kwenda namba 15441 bila kutozwa gharama yoyote na baada ya hapo atapokea ujumbe wa uthibitisho kwamba ana dakika 5 kuanzia muda huo kutumia kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kuperuzi.”
Kupitia promosheni hii wateja na watanzania kwa ujumla pia watapata fursa ya kushuhudia wanamuziki mastaa wa hapa nchini wakishirikiana na wanamuziki wengine Afrika katika msimu wa pili wa kipindi cha Coke Studio Afrika kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC1 na TBC2) kila siku za Jumamosi saa 3 usiku.
Aliongeza kuwa promosheni hii inapatikana kwa wateja wa Vodacom Tanzania nchi nzima. http://kula5.co.tz/