Nyumba zaidi ya saba za kuishi na nane za maduka pamoja na mifugo;
vyote vikimilikiwa na viongozi wa CCM, akiwamo mbunge na madiwani wilayani Liwale, vimeteketezwa kwa moto na kuharibiwa na wahalifu.
Mali hizo zikiwamo za viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ilulu, Liwale, vimeteketezwa kwa kilichdaiwa kuwa ni kupinga kulipwa malipo kidogo ya korosho, msimu wa mwaka jana.
Taarifa ya Polisi, ilisema jana kuwa watu wanaodhaniwa kuwa wakulima wa korosho, walijaribu kuzuia gari lililokuwa na malipo ya korosho, wakipinga malipo ya pili ya zao hilo na kufanya vurugu na uharibifu wa mali.