Aliyekuwa kuwa Mwanasheria wa Kenya Mh.Amos Wako amewataka wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuchukua tahadhari kubwa katika kuiga namna ambavyo nchi zingine zimefanya ili kuweza kupata katiba mpya na siyo kunakili kila jambo…
Mwanasheria huyo mstaafu na ambaye kwa sasa ni seneta wa jimbo la busia mashariki ameyasema hayo alipokuwa akitoa uzoefu wa Kenya kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuhusu mchakato waliopitia katika kufanikisha kupatikana kwa katiba mpya..
Wako amesema kuwa baada ya machafuko ya nchini Kenya na jumuia ya kimataifa kuingilia kati, mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya usuluhishi iliyoongozwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan yaliona kuwa suala la kupata Katiba mpya nchini Kenya, lichukuliwe kuwa suala la Haraka na dharura.