
Watu wawili waliripotiwa kupigwa risasi kwenye show ya J.Cole katika eneo la kupaki magari, wakati wa ziara yake ya “Forest Hills Drive tour” ambayo ilifanyika Holmdel huko New Jersey siku ya Jumatatu Agosti 3, imeripotiwa concert iliishia kwa kupigwa risasi katika eneo la PNC arts Center, taarifa za complex.com zimeeleza.
“Vyombo vya dola viliwahi eneo la tukio baada ya mashahidi kuripoti kutokana na tukio hilonje ya concert ya J.Cole kwenye parking. Habari za tukio hilo pia zilionekana kupitia tweets nyingi zilizopostiwa na watu mbalimbali.
Account rasmi ya New Jersey Fire Alert ilituma tweets mbalimbali kuhusu tukio hilo, kwenye tweet moja, waliripoti kwamba polisi wa New jersey wamethibitisha watu wawili walipigwa risasi.
Ziara ya j.Cole ya “Forest Hills Drive” ambayo pia yupo Big Sean na YG, imeelekea New York City siku ya jana Agosti 4.
J.Cole mwenye ajasema chochote kuhusiana na tukio hilo..
