Albamu ya Girl ni albamu ya pili ya mwanamuziki na mtayarishaji wa mapigo ya muziki Pharrel Williams, Albamu hiyo ilitoka Machi 3, 2014 kupitia lebo yake I Am Other na Columbia Records. GIRL imefuatia albamu yake ya mwanzo ya miaka 8 iliyopita iliyotoka 2008 iliyoitwa In My Mind. Ilikuwa na watu kama Kelly Osbourne, Justin Timberlake, Timbaland, Miley Cyrus, Daft Punk, Jojo, Alicia Keys, Tori Kelly na Leah LaBelle.
Albamu hiyo ilishika namba moja katika nchi 12 duniani pia katika top 10 katika nchi 17 duniani, Girl imeuza zaidi copies 450,000 nchini Marekani Juni 2014.
Ngoma ya Happy inaongoza katika tuzo kibao ikiwa na mafanikio makubwa duniani na imeuza karibu copies milioni 10 duniani kote.Katika albamu hiyo kuna ngoma kama “Marilyn Monroe” na “Come Get It Bae” pia zimekuwa na mafanikio. Ngoma ya Happy ilitoka Novemba 21, 2013, Marilyn Monroe Machi 10, 2014 na Come Get It Bae ilitoka Mei 8, 2014.
Ngoma zinazopatikana katika albamu ya GIRL ni pamoja
1. Marilyn Monroe
2. Brand New (feat. Justin Timberlake)
3. Hunter
4. Gush
5. Happy
6. Come Get It Bae (feat. Miley Cyrus)
7. Gust Of Wind (feat. Daft Punk)
8. Lost Queen
Hidden Track: Freq (feat. JoJo)
9. I Know Who You Are (feat. Alicia Keys)
10. It Girl
11. Japanese Bonus Track: Smile