Amber Rose ameomba talaka kutoka kwa mume wake Boss wa Taylor Gang mkali Wiz Khalifa kwa sababu ameshawishiwa kwamba Wiz Khalifa amekuwa akimdanganya mara kwa mara kwa miezi kadha iliyopita, amekua akitoa sababu ambazo haziingi kichwani.
TMZ imeweka mambo hadharani baada kuona makaratasi Jumatano ambayo yanaonyesha Amber Rose akitaka talaka na kuachana kwao sio kwema kabisa, kila mmoja anamlaumu mwenzake kwa michepuko.
Chanzo kimoja kilicho karibu na Amber Rose kimeiambia TMZ, toka ilipoanza tour ya Wiz Khalifa mwezi Julai, Amber Rose anauhakika Wiz Khalifa amekuwa na michepuko.
Amber anawaambia marafiki, alitaka kuwa kwenye tour hiyo na Wiz Khalifa lakini alimpa sababu kibao ambazo alitaka asiwe na Amber, sababu kubwa kwamba atatakiwa akae nyumbani na mtoto wao mwenye mwaka mmoja anayeitwa Sebastian.
Pia anasema alijaribu kumuonyesha yeye ndio ana nguvu kwa kumwambia alitakiwa aachwe nyumbani yeye aende kutengeneza mkwanja ambao utasaidia familia yao. Hiyo haina mantiki lakini hicho ndicho alichokisema.
Kama ilivyopripotiwa, Wiz Khalifa anaamini kwamba Amber ndiye aliyekuwa akimdanganya, kutokana na Nick Cannon, kwa sasa nay eye katika kujitetea anarudisha majibu kwa kumwambia Wiz ndie mwenye michepuko na kuficha yale makosa yake ambayo Wiz alikuwa akihisi juu ya Amber.
Na kisirisiri Wiz Kahlifa amechukia sana kuhusiana na suala hili…Amber ndiye kupe.