Mtu mmoja mwenye umri katikati sio mzee wa kijana aliyefahamika kwa jina la Onana Osua amepigwa risasi na kufa na polisi baada ya kuwaua watu sita akiwatuhumu kumuwekea sumu kwenye chakula. Tukio hilo limetokea huko Uromi,Esan Kaskazi Mashariki.
Marehemu Osua alisemekana aliondoka hospitali Ambato alikuwa amefikishwa kwa matibabu baada ya kuripotiwa alipewa sumu na kupewa siku 5 za kuishi. Mashahidi walisema Osua alienda nyumbani akachukua bastola yake na kuanza kwenda majumbani mwa watu waliodhaniwa wanahusika na kumpa sumu aliwaua kwa kuwapiga risasi.
Inasemekana Osua alikuwa Mwe yekiti motor park iliyopo Uromi, imefahamika pia alimuua mke akiwa ni mmoja wao aliwasili nyumbani.
Vyanzo vya stori hii vilisema Osu alienda hadi Ubiaja huko ,usini magharibi mwa Esan ambapo aliripotiwa nay eye kupigwa risasi na polisi. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo msemaji wa polisi DSP Abiodun Osifo alisema wahanga wa tukio hilo watatu wamethibitishwa kufari dunia wakati wengine wakiwa katika hali mbaya mbaya hospitalini.
DSP Osifo alielezea kwamba Osua aliwashambulia polisi ambao tayari walishakuwana taarifa za mauaji aliyokwishayafanya kabla ya polisi na wao kumshambulia.
Alisema Osua aliendelea na mauaji kabla ya polisi kumzuia.
The Nation