Mchezaji wa Uruguay Luiz Suarez amefungiwa miezi minne kutojihusisha na shughuli zote za mpira kwa miezi minne kwa kumng’ata beki wa timu ya Italia Georgia Chiellin.
Mchezaji huyo wa Liverpool mwenye miaka 27 pia amefungiwa miezi nane katika mechi za kimataifa, ikianzia katika mechi zote zilizobaki za Kombe la dunia 2014.
Atakosa mechi nane za mwanzo za Ligi kuu ya Uingereza msimu ujao, Uruguay wana siku tatu za kupinga uamuzi huo, Tukio hilo lilitokea Jumanne 2014 katika mechi ya kundi D ambayo Uruguay alishinda na kufuzu katika timu 16 bora. Suarez pia amepigwa faini ya paundi 65,680 sawa na 100,000 Swiss francs.
Adhabu hiyo ni kubwa katika historia ya Kombe la dunia, imepita ile ya Mauro Tassotti wa Italia aliyokosa mechi nane baada ya kumpiga mchezaji wa Hispania Luis Enrique mwaka 1994.
Mechi ya kwanza ya Suarez itakuwa akiwa na Liverpool katika raundi ya nne ya Capital One Cup na mechi zinazotarajiwa kuanza katika wiki ya Octoba 27.
Liverpool atatakiwa ashinde mzunguko wao wa tatu mwezi September kufikia stegi hiyo ambayo Suarez ndo atacheza, Suarez amepatikana na kosa la kuwang’ata wachezaji wa tatu katika maisha yake ya mpira.