
Uwasilishwaji wa rasimu ya katiba uliokuwa ufanywe na mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Mhe.Jaji Joseph Warioba umeshindwa kufanyika baada ya baadhi ya wajumbe ambao ni wanachama wa umoja wa katiba ya wananchi kusimama na kuanza kuzomea kupiga makofi na kuzungumza bila ya utaratibu wa kupinga kuwasilishwa kwa rasimu hiyo kwa kile walichodai kuwa kanuni zimekiukwa.
Kwa upande wa wa wabunge ambao wanaunga mkono kilichotokea bungeni wamesema mwenyekiti ameanza kwa kukiuka kanuni kana kwamba wakati zinapitishwa hakuwepo na hivyo hawawezi kamwe kukubali kuburuzwa..
