
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kwa kuwateua mawaziri na manaibu waziri, kuziba nafasi zilizoachwa na mawaziri wanne waliojiuzulu na mmoja aliyefariki dunia hivi karibuni.
Katika uteuzi huo Rais Kikwete amewateua mawaziri wapya wawili na manaibu waziri wapya wanane, huku akiwapandisha vyeo manaibu waziri wanne kuwa mawaziri kamili.
Miongoni mwa mawaziri wapya ni pamoja na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dokta Asha-rose Migiro, ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria, huku Dk. Titus Kamani akiteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Waziri pekee aliyeachwa katika mabadiliko hayo ni aliyekuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa.
Miongoni mwa manaibu waziri wapya ni pamoja na Juma Nkamia ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mtangazaji, ambaye amepewa dhamana katika Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete yametokana na kujaza nafasi za mawaziri ambao walilazimika kujiuzulu baada ya ripoti ya bunge kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili kubaini kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utesaji na udhalilishaji vikidaiwa kutendwa na watekelezaji wa operesheni hiyo.
Ripoti hiyo iliwalazimisha waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kutangaza kujiuzulu, huku naye waziri wa mambo ya ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi kufuata mkondo huo bila kumwaacha waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Shamsi Vuai Nahodha, na Dr.
Mathayo David Mathayo aliyekuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, kutokana na wizara zao kuhusika katika usimamizi wa operesheni hiyo ambayo iliwahusisha polisi, askari jeshi na walizni wa wanyamapori.
Huku nafasi ya tano katika baraza hilo ikiachwa wazi na aliyekuwa waziri wa fedha, Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipata matibabu.
IKO HIVI
Wizara ya katiba na sheria ni Dk. Asha Migiro huku aliekuwa naibu akiendelea.
Wizara ya makamo wa raisi nchi na Mungano mabadiliko ni kwa naibu amabae ni ALL MWALIMU
Wizara ya fedha waziri ni SAADA MKUYA na naibu wake wapili ni Adamu Malima na MWIGULU NCHEMBA.
wizara ya viwanda na biashara naibu wake ni Janeth Mmbene.
Wizara ya ulinzi waziri ni Hussen Mwinyi.
Mambo ya Ndani ni MATHIAS CHIKAWE.
Wizara ya Afya waziri ni SEIF RASHID naibu wake ni STEVEN KEBWE.
Wizara ya elimu naibu waziri ni JENISTA MUHAGAMA.
Wizara ya maendeleo ya jamii na watoto PINDI CHAMA.
Wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi waziri ni TAITASI KAMANI na naibu ni KAIKA SALIGIGO PELELE mbunge wa Ngorongoro
Wizara ya Ardhi naibu wake waziri ni JOJI SIMBA CHAWENE.
Wizara ya Maji naibu waziri ni AMOSI MAKALA.
Wizara ya Kilimo naibu waziri ni Godfrey MZAMBI.
Wizara ya Habari utamaduni na michezo naibu wazri ni JUMA NKAMIA.
Wizara ya Mali asili na Utali waziri ni LAZARO NYALANDU naibu wake ni MAHAMAD MGIMWA
Wizara ya nishati naibu waziri ni CHARZI KITANGWA.
WIZARA AU NAFASSI AMBAZO HAZIJATAJWA ZIMESALIA BILA MABADILIKO MFANO WAZIRI WA ELIMU BADO NI SHUKURU KAWAMBO
