kada mwandamizi wa CCM, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Ester Bulaya (kushoto) akiwa na na Mbunge wa Jimbo la Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Halima Mdee wakiwapungia wananchi mkono wakati wa mapokezi ya viongozi wakuu wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe walipokuwa wakiingia jijini Mwanza kutokea Uwanja wa Ndege, kuelekea kwenye Uwanja wa Magomeni kwa ajili ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.
Shabiki wa Chadema akiwa na ufunguo wa bandia wenye ujumbe wa ‘Funguo ni M4C’ na nyuma uliandikwa ‘CCM baki na kufuli lako, ufunguo ni M4C’ wakati wa msafara wa kuwapokea viongozi wakuu wa CHADEMA walipokuwa wakiingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Magomeni.
Msafara wa pikipiki ukitoka uwanja wa ndege kuwapokea viongozi wakuu wa CHADEMA walipokuwa wakiingia jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Magomeni.
Mbunge wa Jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga, James Lembeli (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika, wakiwapungia wananchi mikono walipokuwa kwenye msafara wa mapokezi ya Viongozi Wakuu wa Chama hicho wakiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara.