Msanii bora wa muziki wa Reggae Tanzania, DABO (Pichani) amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa, baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa kabisa za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (International Reggae and World Music Awards (IRAWMA).
DABO anawania tuzo hizi katika kipengele cha Mtumbuizaji Mpya Bora, akikabiliwa na ushindani kutoka kwa wasanii MC Norman kutoka Uganda, Alkaline na Kranium kutoka Jamaica na Shatta Wale kutoka Ghana.
Zoezi la kuwapigia kura wasanii hawa kuwawezesha kushinda linaendelea sasa mtandaoni. Link ya kumpigia kura ni: http://www.irawma.com/irawma_vote2014
DABO ametajwa kuwania kipengele cha Best New Entertainer
Kwenye kipengele hicho, DABO anachuana na
* Daniel Bambatta Marley – Jamaica
* MC Norman – Uganda, Africa
* Alkaline – Jamaica
* Kranium – Jamaica
* Shatta Wale – Ghana
Msanii mwingine aliyeingia katika tuzo hizo mwaka huu ni pamoja Na Diamond ambayo yeye yupo kwenye kipengele cha
“Best Africa Song/Entertainer na wimbo wake wa mdogo mdogo ambapo anashindanishwa na wasanii kama
Davido -aye(Nigeria)
Awilolongomba-Bundeke(Drc)
Willy Paul Msafi-Tamatam(Kenya)
Eddy Kenzo-Sitya Loss(Uganda)
Diamond-Mdogomdogo(Tanzania)
Bracket-Mama Africa (Nigeria)