Katt Williams amesema ilichukua dakika 20 kwa polisi kuingia ndani ya club ya usiku ya 1OAK wakati risasi zilivyopigwa kwenye VMA party.
Taarifa kutokana na mchekeshaji Katt Williams, amesema CEO wa zamani wa Death Row Records Suge Knight alikuwa akijaribu kumsaidia mtu mwingine wakati alipopigwa risasi mara sita huko magharibi mwa Hollywood, California wikiendi iliyopita wakati wa MTV Video Music Awards.
Williams alikuwa na Suge Knight wakati akipigwa risasi, ameweka wazi kwamba mjinga t undo ataamini kwamba Suge Knight ndiye aliyekuwa mtu alietakiwa kupigwa risasi, hakutaja jina la mtu ambaye anaamini ndiye aliyekuwa targeted, lakini alimtaja Chriss Brown katika maongezi yake na TMZ. Pia mchekeshaji huyo amelaani maneno ambayo yametapakaa kwamba shambulio hilo lilikuwa likuhusiana na makundi ya wahuni (gang)
Kifo cha Tupac Shakur, Malcom X na Dr. Martin Luther King Jr vilitajwa wakati wa maongezi ya mchekeshaji huyo William.
“Na uhakika Suge anajua nani alimshoot, kama polisi wanasema hakuna mtu aliyemshoot naamini hakuna mtu aliyemshoot, na kama hakuna mtu aliyemshoot basi ni sawa hakuna mtu aliyemshoot Tupac, na kama hakuna mtu aliyemshoot Tupac ni sawa hakuna mtu aliyemshoot MLK. Na kama hakuna mtu aliyemshoot hiyo ni sawa pia hakuna mtu aliyemshoot Malcom X, kumejawa na hakuna hakuna tu” alisema William.
Kufuatia kupigwa huko risasi ambapo ilitokea Agosti 24, Suge Knight alifanyiwa upasuaji kutokana na majeraha aliyoyapata, familia yake imetoa statement kuhusiana na kupigwa risasi.
“Familia ya Suge Knight inakuomba kuendelea kumuombea Suge Knight,kuepuka mambo mabaya mabaya yanayoongelewa na vyombo vya habari, Suge kwa sasa amepumzika ana alipoteza damu nyingi sana, yeye ni binadamu, amefanya mengi kwenye jamii na utamadunu kwa hiyo wote tunatakiwa kuheshimu hilo” statement kutoka kwenye familia ilieleza.