Waziri wa ujenzi Dk. John Magufuli amesimamia ujenzi wa daraja la mto Mziga lililopo Kongowe jijini Dar es salaam ambalo lilisombwa na mafuriko za mvua zinazoendelea kunyesha ambapo limesababisha usumbufu [foleni] kwa abiria wanaokwenda mikoa ya Kusini [Lindi na Mtwara]..
Daraja hilo limesababisha msururu mkubwa wa mabasi yaendayo mikoa ya kusini hali iliyosababisha mabasi hayo kushindwa kufanya safari zake na hata kwa watembea kwa miguu hawakuweza kupita..
kutokana na daraja hilo kubomoka watu walioko upande wa Kongowe na Mbagala hawakuweza kuvuka toka upande mmoja kwenda mwingine.