Siku ya Jumatano 4 Februari 2015 katika hoteli ya New Africa Hotel jijini Dar es salaam, kampuni ya Multichoice ilikuwa na furaha kuzindua king’amuzi kipya cha Dstv HD dikoda ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
King’amuzi hicho kipya kitakuwa na uwezo wa hali ya juu ambacho kitakuwa kinaonyesha picha zenye ubora wa hali ya juu.
King’amuzi cha Dstv HD dikoda, kitakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuonyesha picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1.
Dstv HD dikoda itakuwa na remote yake kwa ajili ya kumrahisishia mteja kuweza kutumia huduma kwa vile anavyotaka kwa ajili ya kufurahia huduma hiyo.
Dstv HD dikoda inapatikana katika ofisi zote za Multichoice pamoja na mawakala wote waliopo Tanzania nzima.
Akizungumzi bei za king’amuzi hicho Meneja Masoko wa Dstv Furaha Samalu amesema “King’amuzi hiki kwa sasa kinapatikana kwa bei ya shilingi 39,000/= tu ikiwa ni ofa maalum itakayoishia Jumapili 8 Februari 2015 wakati mashindano ya AFCON yatakapomalizika, akasema kwa wale wanaotaka kubadilishiwa kupatiwa king’amuzi hiki, watabakiwa na kile cha zamani, ili kupata kipya watalipia shilingi 39,000 ikiwa ni bei rahis kabisa ili wateja wa Dstv waweze kufurahia huduma za Dstv hususani king’amuzi kipya cha Dstv HD ZAPA ambacho ni cha kisasa na chenye ubora wa kisasa muonekano wa picha na sauti bora zaidi”.
Ukinunua king’amuzi hiki cha Dstz HD ZAPA haurudishi kile cha zamani bali unabaki na kile cha zamani unaweza ukampatia ndugu au jamaa ili aendele kufurahia ulimwengu wa Dstv.
Ukiwa na king’amuzi hiki kipya cha Dstv HD ZAPA unakuwa na uhakika wa kuona picha katika ubora wa hali ya juu, pia unakuwa na uwezo wa kurekodi vipindi vyote ambavyo unaona hautakuwa na muda wa kuangalia na ungependa visikupite, zikiwemo series, michezo na vinginevyo vingi.
Akizindua king’amuzi hicho kipya Meneja Uendeshaji wa Dstv Ronald Shelukindo amesema “Dstv HD ZAPA ni king’amuzi kipya cha kisasa ambacho kitakufanya ufurahie picha nzuri pamoja na sauti iliyotulia, pia utaweza kurekodi vipindi vyako unavyovipenda, pamoja na kutega ili usiweze kupitwa na vipindi unavyovipenda ikiwa na kukupa muongozo (guide) wa vipindi vijavyo kwa siku 8 mbele”
Kupitia king’amuzi hiki unaweza kuona channel zote za kitanzania ikiwemo ITV,Channel 10, Tbc na Star TV bila kunatanata (stuck) hili likiwa ni tatizo kubwa wanalokupambana nalo wateja wanapokuwa na vin’gamuzi vingine.
Unaweza kupata muongozo wa vipindi vinavyokuja (Guide) ikiwa pamoja na kukumbushwa (Reminder) kwa ajili ya kipindi chako ambacho usingependa kikupite.
Huduma mpya ya Dstv ni Dstv Now hii inakupa uwezo wa kutazama vipindi vya Dstv popote pale ulipo ukiwa na smartphones, tablets,laptops na vifaa vingine vyenye uwezo kama hivi.
Kwa maisha ya sasa yenye mihangaiko mingi hapa ndipo Reminder Premier Catch Up inapotumika, muda mwingine uko mbali na TV yako na usingependa upitwe na breaking news zinatokea katika Televisheni, unajisajili kupitia App kwa kujisajili kwa kuandika Dstv Now.
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja Mahusiano wa Dstv Barbara Kambogi amesema “Kutoka na teknolojia kukua zaidi ndo maana na Dstv wanakuwa zaidi kuendana na teknolojia inavyokuwa, tofauti na simu za siku za nyuma lakini sasa hivi simu ni za kisasa ambazo unaweza ukafanya kila kitu ni kama uko na kompyuta na kwa hiyo sasa Dstv sasa inaweza kuonekana kupitia simu yako ya mkononi kupitia huduma ya Dstv Now, ukapata kila kitu kinachoendelea kwenye Tv popote pale ulipo”
Huu ndo wakati unapohisi unahisi usingizi hutaki kukaa sebuleni basi utaenda chumbani ukiwa kitandani utaingiza namba jina lako linalotambulika kama mteja pamoja account yako ya Dstv. Utafanikiwa kuangalia Dstv ukiwa chumbani kupitia simu yako, laptop au tablet.
Ili upate huduma hii ni kwamba hakikisha wewe ni mteja wa Dstv ambaye umelipia huduma yako, utatakiwa uingize (Register) jina lako na namba ya account yako ya Dstv ndipo utakapoweza kufaidi huduma hii popote pale ulipo.
Unaweza kutumia huduma hii kwa vifaa hadi vinne kwa wakati mmoja, kupata huduma hii ya Dstv now,angalia App store ili uweze kudownload huduma hii kupitia www.dstv.com kwa watumiaji wa iOs,wakati watumiaji wa Android watapewa nafasi ya kuregister na kuunganisha smartcards kupitia Application hii. Baada ya hapo utaweza kudownload unachokitaka (Favorite Catch Up titles) na kupata unachokipnda ikiwemo supersport,plu M-Net channels za movies ikiwemo Comedy, Actions Plus, Drama na Romance na Premier.
Pia kitu kingine kirahisi kabisa unaweza kutafuta kipindi kwa jina au alfabeti ikikurahisishia kupata kwa haraka unachokitafuta.
Kuna channels zilizotengwa kwa ajili yako uweze kuziangalia kupitia kifaa chako pamoja na kuona vipindi vijavyo vya mbele kwa siku 8 zijazo, hii huduma inapatikana kwa wateja wa Dstv.
Anza sasa kwa kudownload na huo ndo utakuwa mwisho wa kupitwa na vipindi na michezo ambayo usingependa ikupite ukiwa mbali na nyumbani au sehemu ambayo unaweza kutazama telivisheni.
Kufahamu na taarifa zaidi kuhusu Dstv Now App na maunganisho ya huduma za Dstv tembelea www.dstv.com.