
Kendrick Lamar na Kahlil Joseph wameungana kwa ajili ya kufanya filamu fupi ya “m.A.A.d” ikiwa inazungumzia sana sana albamu ya kwanza ya K.Dot ya “good kid m.A.A.d city”.
Filamu hiyo imepangwa kuwa ya dakika 14 na itafanywa kwenye tamasha linalokuja la Sundance taarifa za Fader zilieleza.Joseph ameshinda tuzo ya Sundance na filamu ya “Until The Quiet Comes” aliyofanya kazi akiwa na Flying Lotus.
Good kid m.A.A.d city albamu ya kwanza K.Dot ndo itakuwa story kuu katika filamu hiyo ya dakika 14, filamu imepangwa kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Agosti 9 pale Ace Hotel huko Los Angeles na katika filamu hiyo ataonekana Kahlil Joseph, Tina amepangwa kuperform siku hiyo.
