Hali ya hewa nchini Marekani imezidi kuwa mbaya ambapo majimbo yote 50 ya nchi hiyo yamekumbwa barafu kali. Hali ya hewa hiyo mbaya imesababishwa na hali inayojulikana kitaalamu kama ‘arctic blasts’ imeathiri karibu watu milioni 190.
Katika jimbo la Kentucky, mfungwa mmoja aliyetoroka alilazimika kurudi ili kujinusuru na baridi kali.
Baadhi ya maeneo ya Midwest jotoridi limeshuka na kufikia nyuzi joto – 26C, baridi ambayo inaelezwa kubwa kali zaidi kuliko ndani ya jokofu.
Majimbo yaliyoathirika zaidi ni Alabama,Georgia, Tennessee, Arkansas, Michigan, Maryland, Ohio, Pennsylvania na New York.