
Oscar Pistorious ambaye anatuhumiwa kwa kumuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp, baada ya kudhania ni mwizi aliingia ndani kwake mwaka jana 2013 huko Afrika kusini.
Oscar Pistorious asiye na miguu ameathiriwa vibaya kutokana na ulemavu huo, dakatari wa michezo ameiambia mahakama inayosikiliza kesi hiyo ya mauaji inayomkabili mwanariadha huyo.
Kitu kinachoangaliwa ni akili ya Pistorious wakati akifyatua risasi kwenda kwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Wayne Derman ameiambia mahakama mjini Pretoria kuwa bingwa huyo wa Olimpiki ameathtirika vibaya kutoakana na msongo wa mawazo na hofu.
