Chris Kelly ama Mac Daddy, moja ya artist wa kundi bora kabisa la michano na breakdance miaka ya 90 kutoka Marekani, Kris Kross….. amefariki jana akiwa na umri wa miaka 34.
Msanii huyu alipatikana nyumbani kwake huko Atlanta akiwa amekufa na hili lilithibitishwa baada ya kufikishwa hospitali na kufanyiwa vipimo vya awali.
Taarifa zaidi kuhusiana na kifo cha Mac Daddy zitatolewa hivi karibuni.
Kris Kross inaundwa na Kelly pamoja na Chris Smith ambao walijipatia umaarufu wakiwa na umri wa miaka 13 tu,
na Jermaine Dupri ndio anachukua credits zote kwa kuona kipaji chao na kuwainua, na hivi karibuni walitokezea sana kwa headline baada ya kupanda tena jukaani baada ya kipindi kirefu cha ukimya, mwezi February mwaka huu.
stor Credit: sammisago.com