Wananchi wa manispaa ya Morogoro wamelazimika kutembea kwa miguu kutwa nzima na wengine kutumia usafiri usio rasmi wa Malori na pickup huku wanafunzi wakionekana kuzagaa katika vituo mbalimbali vya magari kufuatia madereva wa daladala kugoma wakilalamikia kukamatwa mara kwa mara na kutozwa faini kubwa na askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani .
Mgomo huo umeonyesha kuathiri wakazi wa manispaa ya Morogoro ambapo baadhi ya wanafunzi wameshindwa kufika mashuleni na baadhi ya wafanyakazi kuchelewa makazi ambapo wakizungumzia hali hiyo wananchi wameiomba serikali kufanya jitihada za haraka ili kuondoa kero ya usafiri ambapo baadhi ya a magari yasio rasmi yameonekana kubeba abiri kwa bei kubwa kati ya shilingi 300 hadi 1000.
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa morogoroDAVID SHILOGILE amesema madereva wamefanya mgomo huo makusudi ili waendelee kuvunja sheria za barabarani na kuongeza kuwa hata waendelee na mgomo watahakikisha wanasimamia sheria za barabarani na atakaye patikana na hatia ya kuvunja sheria za barabarani atachukuliwa sheria..,