
Muimbaji na mwandishi wa nyimbo mkali kutokea Toronto Canada ambae siku za karibuni amekuwa akiandamwa na kesi kibao, ikiwemo ya kumsambulia dereva wa limo huko Toronto Canda mwaka jana mwezi Desemba imefutwa jana kutokana na kukosekana ushahidi uliostahili.
Katika video iliochukuliwa na kamera, simu iliyopigwa ya 911 na polisi kuwahoji mashuhuda ambao polisi walifanikiwa kuongea nao, imeonekana hakuna ushahidi wa kutosha wa kuendeleza kesi hiyo.
Watu walikuwa wamekaa nyuma ya limo, lakini haikufahamika wala kumjua ni nani ambae alikuja kumshambulia mshitaki huyo, mwanasheria David Mitchell aliiambia mahakama.
Mwanasheria na Justin Bieber Brian Greenspan aliwaambia maripota kwamba wameridhishwa na maamuzi hayo yaliyofikia.
“Kweli kabisa ni imani yetu kwamba hakuna mtu aliyemshambulia dereva, hiyo bado inaweza ikawa ni maongezi tu, sehemu yetu ni kwamba hakuna aliyehusiana na Mr Bieber ambaye alifanya kosa hilo” alisema mwanasheria wa Bieber , Greenspan.
Greenspan aliongeza kwamba hawana kitu kibaya dhidi ya polisi ambao walifanya kazi yao kwa kuchunguza shtaka hilo.
