Mbunge wa viti maalum leo amemchachafya Mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2011 Brigitte Alfred baada ya kuibua hoja kuwa mrembo huyo hana sifa ya kuiwakilisha Tanzania Kutokana na kwamba hajui kiswahili,
Mimi Binafsi Niliwahi kufanya maojiano na mrembo huyo kabla hajawa mshindi akiwa mrembo wa kinondoni na ninachokumbuka maelezo yake ni kwamba sio kwamba hajui kiswahili pasee anajua japo anasema hupendelea Kiingereza kwasababu ndio lugha anayoimudu kutokana na kukulia katika mazingira ya Lugha Hiyo Huko Nairobi Nchini Kenya Alipopata elimu yake.
Bi Ruka Ambaye ni mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar alisema ya kuwa Mrembo huyo hastahili kuwa muwakilishi wa tanzania katika mashindano hayo kwakuwa hajui Lugha ya Kiswahili, Huku akipendekeza mashindano hayo kufutwa na kuwekwa mashindano ya sayansi ambayo yatakuwa na faida zaidi kwa jamii.
Cha ajabu kupitia mtandao wa tweeter sehemu ambapo story hiyo iliwekwa kwa Account ya @eastafricaradio Mrembo huyo aliamua kujibu kwa lugha ya kingereza kwa kupost Tweet hiyo ailiyo Capture na kuitupia kupitia ukurasa wake wa Picha Wa InstaGram kwa kuandika
“MEAN WHILEAS OUR COUNTRY SUFFERS FROM 3RD WPRLD PROBLEMS THIS IS BEING DISCUSSED BUNGENI?, I WOUL LOVE TO MEET THIS WOMAN! ASANTE MAMA” Alimalizia
Wakati anajibu swali au maelezo hayo waziri wa Habari Utamaduni Na Michezo Dkt Fenella Mukangara Amesema Mashindano hayo hayawezi kufutwa kwasababu yanafaida sana kwa Taifa Hili hasa kitalii Zaidi.
Hii ni mara ya Pili kwa Muwakilishi huyo wa Tanzania katika mashindano ya Urembo kwa Mwaka 2013 Brigitte Alfred kukutana na kisanga cha kukosolewa kutokana na kutumia zaidi Swaglish hata pale anapohiotajika kuzungumza Kiswahili Baada ya kuzomewa Bungeni Na Wabunge wakati alipokuwa anazungumza bungeni kwa lugha ya kingereza badala ya Kiswahili.