Ni Utama wao kila inapofika mwishoni mwa mwaka ambapo wazazi hawa wawili waliowahi kuoana na sasa wametengana na kubaki katika swala la ulezi wa watoto wao Kimora Lee Simmons na aliywahi kuwa mumewe Russell Simmons kukitana pamoja na kusherehekea msimu wa sikukuuu pamoja na watoto wao
Mama huyo wa watoto watatu ambaye kwa sasa pia ni mtarajiwa wa mtoto mwingine wa nne na mume wake mpya ambaye ni mfanya kazi wa bank Tim Leissner kwa sasa yupo katika katika visiwa vya Caribbean st.Barths akiwa anasherehekea sikukuu za mwishoni mwa mwaka pamoja na Ex Mume Wake Russell watoto wao Aoki, 12,na Ming, 14 pamoja na Kenzo mtoto wake wa miaka 5 alozaa na mcheza sinema Djimon Hounsou.
Chakushangaza mume mpya Wa Kimora Hakuwepo katika bata hilo
Ni hivi tu karibuni Kimora Alipojitokeza kwa mara ya kwanza na kuonyesha ujauzito wake ambao kwa sasa unakadiriwa kuwa tayari wa miezi sita na mume wake mpya
Kimora ni mwanamke anayependa sana watoto hakika kama walivyo mastar wengine kama kina Angelina Jolie, Victoria Beckham , Madona nk