
Tyga na girlfriend wake wa siku nyingi Kylie Jenner imeripotiwa mahusiano yao hatimaye yamegongvukingo, TMZ inaripoti.
Jenner ndiye anayeripotiwa kuvunja mahusiano hayo na Tyga siku ya Alhamisi usiku, kitu kilichosababisha waachane ni msukumo kutoka kwa familia ya Kardashians.
TMZ pia inaripoti kwamba Jenner hakuwa mmoja wa watu waliohudhuria sherehe za kuazimisha siku ya kuzaliwa Tyga juzi Novemba 19.
Wawili hao walikuwa wakisemekana kuwa na mahusiano wakati Jenner akiwa na umri wa miaka 18, waliweka mahusiano yao wazi kipindi hiki cha kiangazi Jenner alipotimiza umri wa miaka 18.
Kylie Jenner anaonekana kwenye video ya ngoma ya Tyga “Stimulated”.
