
Baada ya zile tetesi nyingi katika vyombo mbali mbali vya habari vya marekani hatimae Ciara amewathibitishia mashabiki zake kuwa ni mjamzito kupitia kipindi cha luninga cha ‘The View’ cha jan. 14
Mwanamuziki Ciara mwenye umri wa 28 sasa alithibitisha kwa kuzungumza lakini haikutosha pia akasimama na kuonyesha tumbo laki likiwa na nguo kuwa ni mja mzito kweli na yeye sasa ni mama mtarajiwa Hivyo siara anatarajia mtoto wake wa kwanza na Mchumba Wake FUTURE Mwanamuziki huyo Ciara amekuwa akificha Tumbo lake kwa mavazi anayovaa hata alipokuwa kwenye mahojiano lakini baada ya mtangazaji Barbara Walters kumuuliza kuwa angependa kuthibitisha ua kukataa kuwa ni mjamzito ndiopo aliposimama na kubana nguo yake ili tumbo lionekane Ciara Ni mchumba halali wa Future, Future ana mtoto mwingine kwenye mahusiano yake mengine yaliopiya japo kwa Ciara yeye atakuwa mtoto wake wa Awali Jinsia ya Mtoto bado Haijajulikana wala ni lini kiumbe hicho chatarajiwa kuwasili Duniani
