![](http://salmamsangi.com/wp-content/uploads/2013/04/wpid-janet-jackson-muslim-160x100.jpeg)
Nas anaeleza kufananishwa kwa “good kid m.A.A.d na “Illmatic” asema sio sawa kwa Kendrick Lamar, kwa kuongeza alitoa maoni yake kuhusu repa huyo kutoka Compton Kendrick Lamar wakati akipiga stories na Complex pia alizungumza katika matoleo tofauti ya story iliyotolewa na Complex.
Repa huyo kutoka Queens bridge aliulizwa kuhusu albamu ya Kendrick ya good kid m.A.A.d city na jinsi alivyo na presha kutokana na albamu yake inayokuja, pia alizungumzia albamu yake ya Illmatic na iliyofuata mwaka 1996 ya It was written.
Alipoulizwa kuhusu Kendrick kulinganishwa nae na zaidi ya albamu ya good kid, m.A.A.d city, Nas aliendelea kueleza jinsi anavyomuani Kendrick na kuweka wazi kwa njia yeyote hawezi kuharibu albamu yake inayokuja.
Nas alisema anadhani Kendrick anaweza, kwa njia yeyote, Kendrick hawezi kuharibu kwa sababu mapenzi yake kwa muziki ni makubwa sana, anaweza kufanya ngoma kali na zinakuwa kali nazitakuwa next level.
Kwa hiyo Kendrick yuko katika wakati mzuri kuna wasanii wengi wanaweza kuleta utofauti na kuonyesha umihimu, na Kendrick ni msanii wa aina hiyo, kwa hiyo chochote anachokifanya kwa maoni ya Nas, watu lazima watakoma nazo, hapo hapo hicho ndicho anachotakiwa kukifanya, ni changamoto, maisha ni changamoto na kwenye mchezo wa hip hop ni changamoto.
Baadae Nas aliongelea presha aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma, kwa ukubwa wa kulinganisha ushindani uliokuwepo kipindi cha nyuma.
Nas anasema kipindi kile ushindani ulikuwa mkubwa, Jay Z ndo alikuwa anatoka, ilikuwepo albamu ya kwanza ya Ghostface, alikuwepo Raekwon, walikuwepo Mobb Deep, hawa wote walikuwa wameteka muzuki, bila kumsahau Biggie na wengine wengi, kwa hiyo ushindani ulikuwa mgumu hata kwake kutoa ngoma.
Mwisho Nas akaulizwa kuhusu kulinganishwa albamu yake ya Illmatic na ya Kendrick Lamar ya good kid, m.A.A.d city, alisema sio sawa kulinganishwa kwa albamu hizo kwa sababu good kid, m.A.A.d city ya Kendrick Lamar inawakilisha wakati wa sasa na mambo yanayotokea kwa sasa na Illmatic yake ilikuwa ikiwakilisha kipindi kile cha nyuma, kwa hiyo zina ujumbe kila moja kwa kipindi chake.
Hata aina ya mapigo ya muziki ya kipindi kile yalikuwa tofauti na sasa kwa Illmatic ilikuwa inspired ya mapigo ya muziki kwa kipindi kile na ya Kendrick ipo inspired kwa mapigo ya muziki ya kipindi hiki kwa hiyo sio sawa kuzilinganisha kabisa.
Jinsi biashara ilivyokuwa kwa kipindi kile ukiangalia miaka ile, rap gemu yenyewe ilivyokuwa pia maisha, kwa hiyo albamu ya K.Dot ni mpya ipo kwa ajili ya miaka hii ya sasa.
Unaweza ukazilinganisha kwa sababu unamlingnisha Nas na Kendrick kwa njia nyingi, lakini mwisho wa siku unatakiwa uheshimu safari yake, safari yake ni mpya kumlinganisha na Nas lakini mwisho wa siku ana safari yake mpya mwenyewe kwa kipindi hiki.
Kendrick mwenyewe bado amebaki kimya kutoa taarifa kuhusu albamu yake inayokuja, lazima uwe na presha kwa sababu albamu ya mwanzo ilikuwa kali kwa hiyo unakuja vipi tena ili uweze kuendelea mbele na sio kurudu nyuma, lakini alisema Dr. Dre anafanyia kazi project hiyo mpya.
Kitu kuhusu Dre ni kwamba hawezi kuharibu haimanishi kiasi gani ya pesa alichonacho alipui, kila wakati akifanya kitu lazima kiwe noma akiwa studio lazima afyatue matofali ya kufa mtu Hiyo ni kabla ya deal, baada ya deal, wakati wote anajifungia kuhakisha anatisha…alisema Nas wakati akipiga stories tena na KIIS FM mwezi Juni.
![Top 20 Bongoflava](http://salmamsangi.com/wp-content/uploads/2013/10/Unbenannt.jpg)