Yale majanga aliyoyaimba kupitia wimbo wake wa majanga yamkuta mwenyewe Msanii Snura Baada ya Picha zinazosemekana akiwa kwa mganga anaroga kusambaa katika mitandao mbali mbali ya jamii
baada ya tukio hilo msanii huyo alijikuta akipokea sim nyingi zinazomuhoji nini kimemsibu na haya ndio yake alosema:
Jaman jaman picha zangu zote zilitoka hata sijui nani aliziediti nakubakisha ambazo hazinna camera lakini ukweli ni kwamba ile ilikuwa ni movie nilikuwa nafanya na ni movie ya DOTNATA inaitwa MLOKOLE.
Nashangaa napigiwa simu naulizwa snura umeonekana kwa mganga unaronga kwakweli nilishangaa sana, kuja kuangalia picha naona picha za movie ya Mlokole Nikabaki kucheka tu nikajua ndio mambo ya uhuru wa vyombo vya habari hivyo.
Snura atabaki kuwa snura hawawezi kumshusha hata kwa dawa najua kuna kundi la watu wanatamani sana kunishusha lakini hawawezi kunishusha kwa style hiyo kabisa….
ukiangalia izzo picha kuna uchawi hapo au filamu tu