Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika ya Kusini (Democratic Alliance) kimemfungulia mashitaka ya rushwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma baada ya kutumia fedha za umma kukarabati nyumba yake binafsi.
Mashitaka hayo yanahusishwa na ujenzi wa bwawa la kuogelea pamoja na boma la ng’ombe ambalo limegharimu dola milioni 23.