Jana kupitia mtandao wangi wa InstaGram niliweka picha ya msichana anayesemeka amekamatwa na Madawa nchini Egypt na anatarajia kunyongwa ijumaa hii kama sheria za nchi hiyo zinavyoeleza
kupitia Blog ya wananchi ya Le mutuz hizi ndio picha za msichana huyu akiwa katika pozi mbali mbali, mpaka sasa kuna maelezo mbali mbali yanayoendelea kutolewa kuhusiana na kumfahamu msichana huyu ambae anakwenda kwa jina la Fatma
Msichana fatma akiwa na mwanae
Hii ni screenshot ya video hii hapa chini baada ya kukamatwa kwake na unga, Ingawa habari hizi hatuna uhakika nazo kama ni Mtanzania kama invyodaiwa na wengi au ni mswahili wa Oman kama wengine wanavyodai
Mrembo Fatma maarufu kwa jina la Brown Berry wa mitaa ya Ilala Jijini Dar es salaam haukumiwa kunyongwa mpaka kufa baada ya kupatikana na madawa ya kulevia nchini Misri hukumu ishatolewa na anatakikana kunyongwa ijumaa hii huko huko Misri.
Tufanyaje tumuokoe mrembo Fatma maarufu kwa jina la Brown Berry???? Je ubalozi wa Tanzania Misri unaweza kuongea lolote kuhusu ili?
Maana nchi za wenzetu hawaruhusu jambo hili litokee kwa watu wao utasikia tu wanaandamana wanamtaka mtu wao akaukumiwe nchini kwao je kwanini uongozi wetu unakuwa nyuma kufuatia suala hili? Je inamaana watanzania hatuna dhamani? Natamani angekuja kuadhibiwa huku nyumbani maana mrembo huyu anafamilia na mtoto mdogo anaye mtegemea ata angepata fulsa ya kuacha usiha kwa mwanaye.
Hizi ni coment kutoka mtandao wa InstaGram kwa jinsi watu walivyomuelezea Fatma