
Rais wa mpito wa jamuhuri ya afrika ya kati Michel Djotodia amejiuzulu kufwatia machafuko makali ya kidini ambayo yanaendelea kwa takribani wiki kadhaa nchini mwake.
Rais Michel alikuwa akikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutokana na kushindwa kuthibiti machafuko hayo ya kidini baina ya madhehebu ya kikisto na waislam.
Maelfu ya watu waliandamana leo katika barabara za mji mkuu Bangui kumtaka Rais Djotodia, ajiuzulu.
Rais Djotodia amekosolewa vikali kwa kukosa kumaliza mapigano ya kidini kati ya wakristo na waliokuwa waasi waisilamu ambao walimsaidia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi mwaka jana.
Waasi wa Seleka walifanya mapinduzi mwezi machi mwaka jana na kumteua Michel Djotodia kuwa rais wa kwanza muislam inchini humo.
