Rais wa Uruguay Jose Mujica ameitukana FIFA kutokana na kumfungia miezi minne Luiz Suarez baada ya tukio la kumng’ata mchezaji wa Italia Giorgio Chiellin. Rais huyo mwenye miaka 79 ameelezea adhabu hiyo ni ya kikatili.
Rais huyo anajulikana kwa kuongea wazi bila kuficha vitu, alitoa comment hiyo kwenye Televisheni ya Taifa baada Uruguay kutolewa na Colombia katika timu 16 bora katika kombe la dunia 2014nchini Brazil.
Rais huyo alijifanya kama alichokisema kilimstua kwa kufunika mdomo,alipoulizwa kama alitaka kurekebisha kauli yake, lakini akawaambia waandishi wa habari watoe habari hiyo.
Alisema Suarez alipewa adhabu hiyo kwa sababu ya upole wake siku za nyuma na kusema hiyo ni aibu katika historia ya kombe la dunia.
Oscar Tabarez akiiongoza Uruguay alifungwa 2 – 0 dhidi ya Colombia bila mshambuliaji wake muhimu Suarez katika timu 16 zilizokuwa zimebaki, Chama cha soka cha Uruguay kimesema kitakata rufaakupinga adhabu hiyo.