Waislamu wote duniani leo wanaungana kwa pamoja kusherehekea siku kuu ya Eid baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan ikiwa ni moja ya nguzo 5 muhimu katika Uislamu, takribani mwezi mzima umekuwa ni mwezi wa kumrejea muumba wetu na kuacha madhambi yote yasiyopendeza mbele zake Allah!!
Na tuyaendeleze yale yote tuliyojifunza katika mwezi wa Ramadan, isiwe mambo mema tuyatende katika mwezi mtukufu tu ulioisha bali yaendelee hata hadi mwisho wa maisha yetu hapa duniani!!
Kitaifa ibada ya Eid El-Fitr jijini Dar es salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja!! Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amesali mskiti wa Maamur Upanga jijini Dar es salaam.
Hongera kwa kumaliza salama mwezi mtukufu wa Ramadan na Heri ya siku kuu ya Eid El-Fitr Mungu akujalie afya njema namafanikio tele kwa yote uliyoyaomba katika kipindi cha toba.
Salmamsangi.com inawatakia wote siku kuu njema yenya amani na utulivu mkubwa!!