
Baada ya mkali Chriss Brown kushindwa kutokea kwenye show ya Drake ya OVO Jumatatu, mambo yaliendelea wakatokea wakali kama G.Unit, Lauryn Hill, Outkast na YG ikiwa ni katika siku ya pili ya show hiyo huko Toronto Canada.
Hiyo ni show ya tano ya tamasha la OVO ambayo ilifanyika Jumatatu usiku na kwa mara ya kwanza show imefanyika mara mbili.
Siku ya kwanza ya show Jumapili ilipambwa na Outkast ambao wako kwenye tour yao wakapita kumpa tafu mshikaji wao, walitokea kwenye stage mida ya saa 3 usiku, B.O.B na hitz zote kutoka Stankonia zilitisha kwenye tamasha hilo, Na ngoma zinazopatikana kutoka albamu yao nyingine ya Aquemini ya Outkast ziligongwa ilikuwa ni katikati ya tamasha.
Drake jana amemake headline tena pale Molson Canadian Amphitheater.
