Jumatatu usiku (July 22) Beyonce alikuwa na show huko Montreal, Canada…
Wakati anaimba wimbo wake wa ‘Hallo’ ghafla nywele zake zikanaswa na feni iliyokuwa nyuma yake jukwaani hapo,Kuonyesha kujiamini na uzoefu alionao hakuonekana kutetereka bali aliendelea kuimba huku walinzi wake wakiendelea na zoezi la kutenganisha nywele hizo na feni.
Bey alisimama kwa muda huku wasaidizi wake wakijaribu kukata sehemu ndogo ya nywele zake na mkasi ili aweze kuwa huru na kuendelea na show.
Sasa ndo najiuliza hapa ingekuwaje kama ndio wigi jamani si yangekuwa majanga hayaa lol, ila hii inaonyesha ni jinsi gani wenzetu wako makini maana ajali ni popote so lazima ujipange ili hata ikitokea ajali mambo hayaharibiki sana.
Zoezi la kutenganisha nywele za Mama Ivy Blue Lilifanikiwa na kumuacha bibie aendelee na show yake kama vile hamna kilichotokea.