KATIKA hali isiyo ya kawaida kwa mila zetu waafrica,vijana wawiliTshepo Cameron Modisane na Thoba Calvin Sithole wamefunga Ndoa ya jinsia moja almaarufu kama “GAY MARRIAGE” huko mjini KwaDukuza ulioko KwaZulu-Natal, South Africa na kuwa tukio la kwanza barani Africa kuwahi kutokea.
Habari zaidi zinadai wanandoa hao awali walikuwa na mahusiano ambayo kila mmoja katika mji huo alikuwa akiyatambua….Umaarufu wa uhusiano wao ulisababishwa kituo cha Televion cha KZN ambacho kimekuwa kwa muda mrefu kikiyatangaza mahusiano yao….
“Kwa muda mrefu tumejaribu kuuonyesha uhusiano wetu huu mbele za watu ili wale ambao walikuwa wanajificha na kuogopa waweze kuiga mfano mzuri ambao tumeuonyesha kwani ni kitu kizuri kama umempenda mpenzi wako na kuamua kudhihirisha hilo katika halaiki ya watu ” alisemaTshepo ambaye alionekna kuwa na furaha kupita kiasi na kuongeza:
“Tumeona hakuna haja wa kutokuwepo kwa Ndoa za namna hii huku kwetu(AFRICA), na Ndoa yetu ni Alama kwa ulimwengu kwamba Mashoga wanaweza kuoana na kutengeza familia yenye maadili yote tofauti na watu wanavyofikiria”
Kwa upande wa Thoba , yeye alikuwa na machache: “Hivi ndivyo jinsi ambavyo tumeamua kuwa, na Tumechochwa na maneno mengi ya watu ambao wamekuwa wakipinga Ndoa hii katika bara letu hili la Africa”
Wanandoa hao walimalizia Tukio la kihistoria katika maisha yao kwa mabusu moto moto huku wakishangiliwa na watu lukuki.