Leo Branaba na Amini walikuja katika katika mahojia na kipindi cha Music Xpress Friday Special kinachoruka kila Ijumaa saa mbili mpaka saa mbili na nusu channel Ten kwa ajili ya kutambulisha wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la “Why Mimi”
Barnaba Na Amini pia walijitambulisha kama kundi linalotambulika kwa jina la “Gemina” na sasa wanafanya kazi kama kundi japo pia wakati mwingine kila mmoja anasimama kama solo katika kutoa single yake.
Katika Mahojiano yao walieleza mengi kuhusiana na mradi wao mpya lakini jambo la kustusha zaidi maelezo yao yanaonekana hawapo tena chini ya Nyumba ya vipaji Tanzania THT..
Hapa ni Barnaba Na Amini wakiwa na baadhi ya wafanya kazi wa Magic Fm Alen Pitter Kasiga wa pili kushoto na Musa kipanya wa kwanza kulia pamoja na meneja wao mpya waliomtambulisha kwa jina la Mosses wa kwanza kushoto
Mahojiano haya yataruka channel Ten siku ya ijamaa ijayo ya tarehe 19/07/2013 saa mbili kamili usiku
On set
Usikose kutazama kipindi hiki upate kuyasikia yote waliyozungumza