
Mwezi Agosti 14 mwaka huu Lil Wayne alionyesha cover art ya albamu yake inayotoka leo ya The Carter V, Cover art hiyo kwa mara ya kwanza ilitoka kupitia ESPN Sports Center ikiwa ina picha ya mama yake.
“Ni vizuri, kila wakati imekuwa ni picha yangu, nilitaka nionekane na mama yangu kwenye albamu hii, kuwa na mama pale ni zaidi ya kushinda, ni mafanikio” alisema Lil Wayne.
Alisema hakumuacha mama yake ajue alikuwa akitumia picha na kweli mama yake hapendi, Wakati akifanya mahojiano na ESPN, Wayne pia ameweka wazi kwamba albamu imepangwa kutoka leo Oktoba 28, 2014.
Mwezi Mei mwaka huu Lil Wayne alisema yafuatayo kuhusu albamu hiyo.
“Mawazo yangu ni ya busara, bado nasema nachotaka kusema, iko fresh na inaleta maana zaidi, yote hayo yanakuja kwa kuwa nimekuwa” .
