Kuna Haja ya Rais Museven Kutafakari upya juu ya uauzi wake wa kupitisha sheria ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja Nchini Uganda Swala hili limepelekea kuzorota kwa Misaada kutoka nchi wahisani Duniani, pamoja na Taasisi Kubwa za kutoa misaada katika nchi inayoendelea kama Uganda.
Haya Yanathibitika Tena Baada ya Benki Ya Dunia Nayo Kutafakari upya Juu ya Kuendelea kuitolea misaaada katika nchi ya Uganda Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuishinisha sheriua mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali. Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola. Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.
Chanzo: BBC